Madaktari wa
Tanzania katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete, wakishirikiana na wenzao wa India wamefanikiwa kufanya
upasuaji wa moyo wa aina yake Tanzania.
Upasuaji huo ujulikanao
kama ‘bypass surgery’ ulishirikisha kupandikizwa kwa mishipa ya damu
kutoka sehemu nyingine ya mwili moyoni bila kutumia mashine ya
kusimamisha moyo na mapafu.Kwa kawaida madaktari wanasema upasuaji wa moyo hufanyika baada ya moyo na mapafu kusimama, lakini upasuaji huo ulifanyika wakati moyo na mapafu vikifanya kazi.