- Fahamu wateja wananua kwa wakati gani
Kuna misimu ambayo wateja huwa wananua zaidi kwa mafano kwa mtu anayefanya biashara ya nguo wateja huwa wananua zaidi kipindi cha mwisho wa mwaka (kukaribisha mwaka mpya) na vipindi vingine ambavyo huwa wateja wananua zaidi hivyo yakupasa kama wewe ni mjasiliamali kufanya juhudi za kua na mzigo mkubwa zaidi.
- Fahamu wateja kwa makundi yao
Mjasiliamali anapofanya biashara hukutana na wateja wa kila aina kwa mafano kuna wateja walemavu, wateja wa dizani hii wanahitaji huduma kama wateja wengine kwa kuwa wewe kama mjasiliamli unahitaji kuuza bidhaa na huduma hivyoo usibagua aina ya mteja. Kundi lingine la wateja ni wateja waulizaji, hii ni aina ya wateja ambao huuliza kila aina ya bidhaa lakini wewe kama mjasiliamali unatakiwa pia kuwahudumia wateja wa aina hii kwa kuwa hawa ndio hutangaza bidhaa na huduma unazouza siku zote kwa kwenda kusimulia kwa ndugu zao jamaa na marafiki. Aina nyingine ya wateja ni wateja wadadadisi, aina hii ya wateja unahitaji kuwa nao makini kwa kuwa mara zote huwa wanaufahamu na bidhaa au huduma wanayohitaji hivyoo unatakiwa kuwahudumia ukiwa na umakini wa hali juu kwa kuwa ukiwadanganya unaweza kuwapoteza aina hii ya wateja.
Imeandaliwa na Mzalendo Mweusi Blog
0 comments:
Post a Comment