Katika
makala hii tunaanza na kuelezea maana ya fasihi, fasihi fasihi simulizi
kwa kutumia wataalam mbalimbali, baada ya kuelewa vizuri dhana hizi
tutajadili vigezo vilivyotumika katika mgawanyo wa tanzu na vipera vya
fasihi simulizi katika makala ya M.M Mulokozi (1989) na hatimaye
tutaangalia ubora na udhaifu wa uainishaji wa tanzu hizo, na kumalizia
na hitimisho, kielelezo na mwisho marejeo.
Fasihi
ni sanaa itumiayo lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii bila kujali kuwa
imeandikwa au haijaandikwa. Fasihi ambayo haijaandikwa ni fasihi
simulizi na fasihi iliyoandikwa ni fasihi andishi.
Ama
kuhusu Fasihi simulizi, Wamitila ( 2002) anaeleza kuwa Fasihi simulizi
ni fasihi ambayo huwasilishwa kwa njia ya mdomo kwa kusimuliwa, kuimbwa ,
kutongolewa au kughanwa.
Naye
Mulokozi (1996) anaelezea kuwa fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au
kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa njia ya mdomo na vitendo bila
maandalizi.
Kwa ujumla fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo na vitendo bila maandishi.
Katika
makala ya M.M Mlokozi (1989) katika mulika ya 21 amejaribu kuzigawa
tanzu za fasihi simulizi ya Tanzania katika tanzu zake mahususi kwa
kuzingatia VIGEZO vifuatavyo;
Umbile na tabia ya kazi inayohusika;upande
wa umbile na tabia ya kazi ya sanaa ameangalia vipengele vya ndani
vinavyoiumba sanaa na kuipa mwelekeo au mwenendo ilionao.Vipengele hivyo
ni namna lugha inavyotumika(kishairi,kinathali,kimafumbo,kiwimbo,
kighani nakadharika) pia muundo wa fani hiyo na wahusika kama wapo.
Kigezo cha pili ni muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira (hili
linazingatia pia dhima yake kijamii) hapa Mulokozi amezingatia ukweli
wa msingi kuwa fasihi simulizi ni sanaa inayo pita, isiyofungwa katika
umbo maalum, wala matini maalum yasiyo badilika. Fasihi simulizi
inatawaliwa na vitu muhimu vitatu yaani watu, wakati na mahali.
Mwingiliano huu ndio muktadha, na muktadha ndio unaamua fani fulani ya
fasihi simulizi ichukue umbo lipi? Iwasilishe vipi kwa hadhira, kwenye
wakati na mahali hapo.
Zifuatazo ni tanzu na vipera vya fasihi simulizi kama zilivyoainishwa na M.M.Mlokozi(1989)
katika mulika 21 na jinsi alivyo ziainisha kwa kutumia vigezo hivi
viwili, yaani kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika na kigezo
cha muktadha na namna ya uwasilishwaji kwa hadhira, na vipera vyake.
M.M.Mulokozi ameainisha tanzu sita ambazo ni; mazungumzo, masimulizi, maigizo (drama) ushairi semi na ngomezi (ngoma). Hivyo
ufuatao ni uainishaji wa tanzu hizi za fasihi simulizi na vipera vyake
kwa kutumia vigezo vya Mulokozi katika mulika ya 21.
Mazungumzo,
ni maongezi au maelezo ya mdomo katika lugha ya kawaida, juu ya jambo
lolote lile. Si kila mazungumzo ni fasihi mazungumzo ili yawe fasihi
lazima yawe na usanii wa aina fulani, na uhalisia baada ya kuunakili.
Tanzu zinazoingia katika fungu la mazungumzo; Hotuba, Malumbano ya watani, Ulumbu, Soga na mawaidha. Katika kuainisha tanzu hizi ndani ya mazungumzo M.M. Mulokozi
ametumia vigezo vyote viwili; Hotuba, malumbano ya watani, ulumbu, soga
na mawaidha. Kwa kuzingatia kigezo cha kwanza kinachozingatia msingi wa
umbile na kazi inayohusika, tunaona tanzu hizi zote zina vipengele vya
vinvyoumba sanaa na kuipa muelekeo au mwenendo ulionao, katika hotuba,
malumbano ya watani, ulumbu, soga na mawaidha vyote vinavipegele vyake.
Pia tanzu hizo zote zina maana ya lugha inayotumika. Mfano katika hotuba
lugha rasmi ndiyo inayotumika, katika malumbano ya watani lugha ya
kejeli mara nyingi ndio hutumika zaidi, mawaidha hutumia lugha rasmi au
lugha za kikabila hutumika.
Pia
katika kigezo umbile na tabia ya kazi inayohusika,katika kuainisha
tanzu hizi mulokozi ametumia muundo wa fani na wahusika kama wapo.Tanzu
zote hizo katika mazungumzo zina fani yake. Mfano katika malumbano ya
watani ni tanzu inayozingatia fani zifuatazo; Kuna utani wa mababu,
mabibi na wajukuu, utani wa mashemeji, utani wa kikabila na utanu wa
marafiki. Kila kimojawapo kati ya fani hazi huwa na kanuni zake,
miktadha yake na mipaka yake katika jamii zinazohusika.
Pia
katika kuanisha tanzu za mazungumzo Mulokozi ametumia kigezo chake cha
pili yaani kigezo kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishwaji
wake kwa hadhira hili linazingatia pia dhima yake katika jamii kama
ifuatavyo;
Ndani
ya mazungumzo kuna hotuba, mawaidha, ulumbu, malumbano ya watani, soga;
Tanzu hizi zote zinazingatia msingi wa fasihi kuwa ni sanaa inayopita,
isiyofungiwa katika umbo maalum, wala matini yasiyobadilika. Mfano
Hotuba ni sanaa inayopita, isiyofungwa katika umbo maaluma na matini
yake hubadilika kulingana na matukio kama vile; matukio ya kidini,
sherehe na kadharika. Hotuba hufuata wakati, watu na mahali. Katika
kigezo hiki kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa
hadhira huzingatia wakati, watu na mahali.Tunaona katika mazungumzo na
tanzu zake zinazingatia wakati watu na mahali, mfano mawaidha huzingatia
watu gani,wana umri gani, je ni vijana wa kiume au wa kike. Pia
huzingatia mahali yaani tukio linapofanyika, mfano sebuleani au chumbani
na pia wakati gani asubuhi, mchana au jioni.
Tanzu
ya mazungumzo kwa ujumla imeainishwa kwa kutumia vigezo vyote viwili
yaani kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohusika na kigezo
kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira.
Masimulizi; ni fasihi yenye kusimulia habari fulani. Mulokozi
(1989) anasema kuwa masimulizi ni fasihi ya kihadithi na fani zake huwa
na sifa zifuatazo; hueleza atukio katika mpangilio fulani mahsusi, huwa
na wahusika yaani watendaji au watendwaji katika matukio yanayosimulia,
hutumia lugha ya kimaelezo, utambaji wake au utoaji wake huweza
kuambatana na vitendo au ishara, na huwa na maudhui ya kweli au ya
kubuni na yenye mafunzo fulani katika jamii.
Katika mulika 21 Mulokozi amegawanya masimulizi katika tanzu zifuatazo; za kihadithi na Tanzu za Kisalua.
Katika tanzu za kihadithi amezigawa katika makundi yafuatayo;
Ngano ni
hadithi za kimapokeo zitumizo wahusika kama wanyama,miti na watu
kuelezea au kuonya kuhusu maisha.Utanzu huu unajumuisha fani kadhaa kama
vile; istiara,mbazi,na kisa.
Tanzu za kisalua zimegawanywa katika fani zifuatazo; visakale, tarihi, visasili,.
Hivyo tunaona kuwa katika uainishaji wa tanzu hii ya masimulizi
mulokozi ametumia vigezo vyote viwili kama ifuatavyo; katika msingi wa
umbile na tabia ya kazi inayohusika Mulokozi ameonyesha vipengele vya
ndani vinavyoiumba sanaa na kuipa mwenendo ulionao. Na vipengele hivyo
ni kama; lugha ya kimaelezo, maudhui, matukio na wahusika.Pia ameonyesha
namna lugha inavyotumika mfano. Ngano hutumia lugha ya kimaelezo na
visakale, mapisi, tarihi, kumbukumbu na visasili. Vipera hivi vyote
hutumia lugha ya kimaelezo.
Pia
katika msingi wa umbile na kazi inayohusika, kigezo hiki huzingatia
muundo wa fani na wahusika kama wapo.Tanzu ya masimulizi ina fani
zifuatazo kutokana na Mulokozi. Hueleza matukio katika mpangilio fulani
mahususi, huwa na wahusika yaani watendaji au watendwaji katika matukio
yanayosimuliwa, utambaji au utoaji wake huweza kuambatana na vitendo au
ishara, huwa na maudhui ya kweli au ya kubuni na yenye mafunzo fulani na
hutumia lugha ya kimaelezo.
Semi ni
tungo au kauli fupifupi zenye kubeba maana fulani au mafunzo muhimu
katika jamii, Mulokozi ameaimisha tanzu za semi kama ifuatavyo:-
Methali ni
semi fupi fupi zenye kueleza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito
yaliyotokana na uzoefu wa jamii. Methali huwa na sehemu mbili kwanza
sehemu ambayo huanzisha wazo fulani sehemu ya pili ambayo hulikanusha au
kulikamilisha wazo hilo. Methali ni utanzu tegemezi ambao kutokea kwake
hutegemea fani nyingine mfano maongezi, majadiliano mazito, muktadha
maalum katika methali Mulokozi ameainisha tanzu hii kwa kutumia kigezo
cha umbile na tabia ya kazi inayohusika, katika kigezo hiki Mulokozi
ameonyesha matumizi ya lugha. Mfano methali hutumia tamathali, sitiari
na mafumbo. Pia methali huwa na wahusika wa fani zake zinazojitegemea.
Mfano Haraka haraka / Haina Baraka. Wahusika kuna anayeuliza Haraka haraka na anayejibu Haina Baraka. Pia lugha aliyotumia katika methali hii ni lugha ya kinathari na kishairi.
Pia
methali huwa na fani zake. Mulokozi anasema methali ni utanzu tegemezi
ambao kutokea kwake hutegemea fani nyingine, fani hizo ni maongezi au
majadiliano mazito, muktadha maalumu, huwa na sehemu mbili sehemu ya
kwanza ambayo huanzisha wazo fulani na sehemu ya pili ambayo
hulikamilisha au kukanusha wazo hilo.
Ndani
ya kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishaji methali huwa na dhima
ya kutoa mafunzo, kuadibisha, kuonya na kuhamasisha jamii. Methali
huendana na wakati, watu na mahali kwa kuzingatia tukio pia huwa na
matini yanayobadilika. Mfano Haraka haraka haina Baraka, methali hii inatoa onyo kuwa ukifanya jambo kwa haraka unaweza kukosea, hivyo polepole ndio mwendo.
Vitendawili; hizi ni
usemi uliofumbwa ambao hutolewa kwa hadhira ili waifumbue. Fumbo hilo
kwa kawaida huwa linafahamika katika jamii hiyo na mara nyingi lina
mafunzo muhimu kwa washiriki mbali na kuwachemsha akili zao. Vitendawili
hutegemea uwezo wa kutambua, kuhusisha na kulinganisha vitu vya aina
mbalimbali vilivyomo katika maumbile, ni sanaa inayojitegemea,
inayotendwa na ina jisimamia yenyewe.
Katika
kigezo cha umbile na tabia inayohusika vitendawili hutumia lugha ya
mafumbo na huwa na washiriki yaani wahusika ambao ni yule anayetoa
kitendawili na anayejibu. Mfano Mmoja huuliza Kitenawili na mwingine anajibu tega. Mfano; Kaa huku na mimi ni kae kule tumfinye mchawi (kula ugali), Mfano huu huhamasisha ushirikiano baina ya watu.
Pia
vitendawili huwa na fani kama wahusika (pande mbili) wanaouliza na
wanaojibu, muktadha maalumu (mazingira) katika muktadha na namna ya
uwasilishaji Mulokozi amesema vitendawili huwa na mafunzo fulani zaidi
ya chemsha bongo. Vitendawili huzingatia mazingira (mahali) watu na
wakati maalum mfano watoto, mahali (shuleni au nyumbani) na huwa na
wakati maalum.
Misimu,
ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea
mazingira maalum. Msimu ukipata mashiko ya kutosha katika jamii hatimaye
huingia katika kundi la methali za jamii hiyo. Mfano Tamu tamu mahonda ukinila utakonda.
Katika
kigezo cha muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira misimu ni
sanaa inayopita isiyofungiwa katika umbo maalum wala matini maalum
yasiyobadilika. Misimu ina dhima ya kutoa mafunzo, kuonya, hutumika
katika siasa pia misimu huenda na wakati, watu na mahali. Mfano Matteru
(1987) anasema ‘tamu tamu mahonda ukinila utakonda’ . Katika mfano
huu unaonyesha madhara ya pombe iliyokuwa inatengenezwa na kiwanda cha
mahonda (Zanzibar). Katika kigezo cha umbile na tabia ya kazi
inayohusika misimu hutumia lugha isiyosanifu kwani huzuka na kutoweka
mfano; mdebwedo, utajiju, yeboyebo, buzi na kimeo.
Mafumbo
ni semi za maonyo au mawaidha ambazo maana zake ni za ndani na
zimefichika. Fumbo hubuniwa na msemaji kwa shabaha na hadhira maalum
hivyo ni tofauti na methali ambazo ni semi za kimapokeo. Katika kigezo
cha muktadha na namna ya uwasilishwaji mafumbo huwa na dhima ya kutoa
maonyo na mawaidha kwa jamii kwani hubuniwa kwa hadhira maalum. Mfano ‘Mbele ya bata kuna bata na nyuma ya bata kuna bata, jumla nina bata wangapi’? Fumbo
hili huonyesha umakini katika katika kufanya kitu. Katika mafumbo ndani
ya kigezo cha umbile na tabia ya kazi inayohisika huangalia namna lugha
inavyotumika, katika mafumbo ambayo maana yake ya ndani imefichika
mafumbo huundwa na wahusika na fani yake. Mfano yule anayetoa fumbo (anasema fumbo mfumbie mjinga ) Yule anayejibu (mwerevu ataling’amua)
hapa anamainisha mjinga hawezi akalifumbua fumbo ila mwerevu hulifumbua
pia mjinga anaweza akadanganywa ila mwerevu hawezi kudanganywa. Fumbo
hili linahamasisha mtu afanye juhudi katika mambo ili afanikiwe kama
mwerevu.
Lakabu
ni majina ya kupanga ambayo baadhi ya watu hupewa au kujipatia kutokana
na sifa zao za kimwili, kinasaba, kitabia au kimatendo. Majina haya
huwa ni sitiari. Majina haya huweza kumsifia mtu au kumkosoa. Mfano Mkuki uwakao – Jomo Kenyatta, Sakarani – mlevi, Simba wa yuda – Haile sellasie.
Katika
kigezo cha umbile na tabia inayohusika Mulokozi ameonyesha lakabu
hutumia maneno yenye maana iliyofungwa na sitiari, pia lakabu huwa na
wahusika yule anayepewa sifa. Mfano mkuki uwakao – Jomo Kenyatta na
anayetoa sifa.
Katika
muktadha na namna ya uwasilishaji lakabu huwa na dhima mbalimbali kama
kusifia, mfano baba wa taifa, inatoa sifa ya utendaji bora wa kazi,
simba wa yuda inaonyesha mshupavu. Mkuki uwakao inaonyesha kiongozi mchapa
kazi. Pia lakabu hukosoa na kuonya mfano sakarani- ulevi hapa
inaonyesha kuwa mtu mlevi hafai katika jamii. Lakabu huwa na matini
yanayobadilika, hivyo ni sanaa inayopita, lakabu hufuata watu wakati na
mahali.
Ushairi,
ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo mashairi na tenzi. Zaidi
ya kuw na vina ushairi una ufasaha wa kuwa na maneno machache au
muhtasari mawazo na maono ya ushairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu.
Mulokozi (1989) anasema ushairi hupambanuliwa na lugha ya kawaida kwa
kutumia lugha na mbinu za kimuktadha. Kauli za kishairi hupangwa kwa
kufuata wizani maalumu na mawimbi ya sauti na mara nyingi lugha ya mkato
na mafumbo hutumika ushairi una fani zinazoambatana na muziki wa ala na
wakati mwingine hupata wizani wake kutokana na mapigo ya muziki huo wa
ala. Mulokozi (1989) amegawa ushairi katika mafungu mawili ambayo ni nyimbo na uwasilishaji.
Nyimbo ni
kila kinachoimbwa hivyo hii ni dhana panainayojumuisha tanzu nyingi za
kinathari kama vile hadithi huweza katika kundi la nyimbo pindi
zinapoimbwa . Vipera vya
nyimbo ni tumbuizo, bembea, kongozi, nyimbo za dini, tenzi, tendi,
mbolezi, kimai, nyiso, nyimbo za vita, nyimbo za uwindaji, nyimbo za
taifa, nyimbo za watoto na nyimbo za kazi.
Katika kuainisha tanzu hiii ya nyimbo Mulokozi ametumia
vigezo vyote viwili, tukianza na kigezo cha kwanza ambacho ni umbile na
tabia ya kazi inayohusika Mulokozi ameonyesha jinsi vipengele vya ndani
vinavyoiumba sanaa na kuipa mwelekeo. Vipengele vilivyo katika nyimbo
ni namna lugha inavyotumika .
Mfano: nyimbo za maombolezo hutumia lugha za maombolezo yenye maneno ya Kufariji tofauti na nyimbo za sherehe huwa na lugha ya furaha na kuchangamsha.
Katika kigezo hiki pia cha umbile na tabia ya kazi inayohusika Mulokozi ameonyesha muundo wa fani na wahusika katika nyimbo. Mfano:
mambo muhimu yanayotambulisha nyimbo ( fani ya nyimbo) Muziki wa sauti
ya muimbaji au waimbaji( wahusika), Muziki wa ala (kama ipo), Matini au
maneno yanayoimbwa,Hadhira inayoimbiwa,Muktadha unaofungamana na wimbo
huo mfano sherehe, ibada na kilio.
Pia
Mulokozi katika kuainisha tanzu ya nyimbo ametumia kigezo cha pili
yaani muktadha na namna ya uwasilishwaji wake kwa hadhira katika
kuainisha tanzu hii ya nyimbo amezingatia wakati, watu (wahusika) na
mahali. Pia nyimbo ina matini yanayobadilika, yasiyofungiwa katika umbo
maalumu yaani ni sanaa inayopita.
Mfano:
kuna nyimbo zinazoimbwa kwa kufuata wakati wake, mahali mahususi, na
mahali maalumu, mfano wawe na vave hizi ni nyimbo za kilimo, mbolezi
hizi ni nyimbo za kilio au maombolezi. Mbolezi huimbwa wakati maalumu,
na waombolezaji ambao ni watu( wahusika) na mahali maalumu (mfano
msibani)
Maghani
ni ushairi unaotolewa kwa kalima badala ya kuimbwa. Zipo maghani za
aina mbili, kuna maghani ya kawaida, ambayo huundwa na fani mbalimbali
za ushairi simulizi mfano mapenzi, siasa, maombolezo, kazi za dini na
kadhalika. Maghani ya masimulizi hutambwa ili kusimulia hadithi,
historia au matukio fulani ambayo huambatana na nyimbo. Tanzu za maghani
ni sifo, vivugo, tondozi, rara, ngano na tendi.
Maghani
ni tanzu iliyoanishwa kwa kutumia kigezo cha muktadha na namna ya
uwasilishwaji wake kwa hadhira. Molokozi ameonyesha maghani huwasilishwa
kwa kalima badala ya kuimba, pia dhima za maghani ni kufikisha ujumbe
kwa hadhira kwa kuzingatia matukio
Mfano uhuru kesi za mauaji
Mulokozi
anasema maghani huundwa na fani mbalimbali za ushairi simulizi mfano
mapenzi, siasa, maombolezo, kazi na dini. Zifuatazo ni fani za ushairi
simulizi ambazo ni, Masimulizi hutolewa kishairi, huhusu matukio muhimu
ya kihistoria au jamii, huelezea habari za ushujaa na mashujaa,
huwasilishwa kwa kughanwa (ala ya muziki), hutungwa papo kwa papo.
Pia
maghani huwa na wahusika, na huambatana na muziki wa ala. Mulokozi
anasema mutambaji wa ghani hizi huitwa Yeli au Manju na kwa kawaida huwa
ni bingwa wa kupiga ala fulani ya muziki (mtambaji huyu ndiye mhusika
mkuu)
Maigizo,
(drama) ni sanaa inayotumia watendaji kuiga tabia au matendo ya watu na
viumbe wengine ili kiburudisha na kutoa ujumbe fulani. Maigizo ni sanaa
inayopatikana katika makabila mengi. Mulokozi anasema drama (maigizo)
ya kiafrika huambatana na ngoma mtambaji wa hadithi au matendo ya
kimila. Kwa mfano jando na
unyago , yapo maigizo yanayofungana na michezo ya watoto, uwindaji ,
kilimo, na kadhalika. Drama hutumia maleba maalumu kama vizuizui (mask).
Katika
kuainisha tanzu hii mulokozi ametumia vigezo viwili,kwa kuanza na
kigezo cha kwanza Mlokozi ameainisha,mambo na vipengele vinavyopatikana
ndani ya maigizo ambavyo ni maigizo yanayohusu matendo ya kimilana
michezo ya watoto,matanga, uwindaji, kilimo na nyinginezo.
Kwa
msingi wa umbile na tabia inyohusika vipengele vya ndani vinavyoiumba
sanaa na kuipa muelekeo tanzu hii ya maigizo ni lugha inavyotumika
katika kuigiza fani na wahusika mfano wahusika wa maigizo wapo na hawa
ndio watendaji wakuu katika kufikisha ujumbe. Maigizo hutumia lugha
mfano lugha ya kejeli na hata lugha rasmi pia maigizo huwa na fani
inayotendwa.
Mulokozi
Pia katika kuainisha tanzu hii ya maigizo ametumia kigezo cha pili
kinachozingatia muktadha na namna ya uwasilishaji wake kwa hadhira,
maigizo ni sanaa inayopita isiyofungiwa kaika umbo maalum wala matini
yasiyobadilika ila maigizo hubadilika kutokana na tukio linaloigigwa na
kuzingatia wakati, watu na mahali mfano maigizo huhitaji sehemu maalumu
(jukwaa au uwanja wa kutendea) , wahusika ambao ndio waigizaji wakuu na
pia maigizo huenda na wakati
0 comments:
Post a Comment