Thursday, 27 October 2016

Matokeo: MATOKEO YA DARASA LA SABA 2016/2017 HAYA HAPA

Bonyeza hapo chini ili kuona matokeo ya darasa la saba. (PALIPOANDIKWA MATOKEO HAYA HAPA)

Sunday, 24 July 2016

Jifunze Kilimo Bora cha Vitunguu

Vitunguu ni zao la pili ambalo hutumika karibu kila siku katika mlo wa familia za kitanzania. Afrika Mashariki, na Dunia Nzima. 
Vitunguu vina chukua nafasi kubwa katika matumizi ya mboga hasa kwa wakazi wa mijini. Vitunguu hutumika katika kutengeneza kachumbari, kiungo cha mboga, nyama na samaki. Majani ya kitunguu hutumika kama mboga. Vitunguu pia hutumika kutengeneza supu n.k

Aina Za kilimo Cha Vitunguu
Kilimo cha vitunguu kinaweza kufanyika kwa aina mbili
  •   Green House
  •  Shambani 
Kilimo cha kitunguu Green House
Kilimo cha vitunguu katika shamba la kawaida.

COMPUTER TROUBLESHOOTING TRICKS

 
My friend fix computers for a living, but the thing he hated the most was to go to the client’s home especially at odd times, carrying kits all around town. Luckily, nowadays this issue is not as irksome as it used to be, the Internet makes the job of the computer geek much easier.

To successfully fix a computer remotely, a few portable programs, some screen sharing apps and a sturdy Internet connection is all you need. With these tools we can offer assistance anywhere in the world pretty much on anything software based. Also, from my experience, fixing computers remotely, can make you very popular as everyone thinks you are a computer genius, capable of doing almost anything, something like a “Computer Champion of Capua”.

Monday, 4 July 2016

MGAWANYO WA TANZU NA VIPERA VYA FASIHI SIMULIZI.

 
Katika makala hii tunaanza na kuelezea maana ya fasihi, fasihi fasihi simulizi kwa kutumia wataalam mbalimbali, baada ya kuelewa vizuri dhana hizi tutajadili vigezo vilivyotumika katika mgawanyo wa tanzu na vipera vya fasihi simulizi katika makala ya M.M Mulokozi (1989) na hatimaye tutaangalia ubora na udhaifu wa uainishaji wa tanzu hizo, na kumalizia na hitimisho, kielelezo na mwisho marejeo.
Fasihi ni sanaa itumiayo lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii bila kujali kuwa imeandikwa au haijaandikwa. Fasihi ambayo haijaandikwa ni fasihi simulizi na fasihi iliyoandikwa ni fasihi andishi.
Ama kuhusu Fasihi simulizi, Wamitila ( 2002) anaeleza kuwa Fasihi simulizi ni fasihi ambayo huwasilishwa kwa njia ya mdomo kwa kusimuliwa, kuimbwa , kutongolewa au kughanwa.
Naye Mulokozi (1996) anaelezea kuwa fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa njia ya mdomo na vitendo bila maandalizi.
Kwa ujumla fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa njia ya masimulizi  ya mdomo na vitendo bila maandishi.

Saturday, 2 July 2016

Futa haya ili kuwa na Whatsapp mbili kwenye simu moja(Two whatsapp accounts on one a

 
1.Unistall Whatsapp ya mwanzo kabisa(official one) then unaenda kwenye folder la whatapps una edit na kuwa OGwhatsapp
2.Nenda kwenye playstore then download OGWhatsapp kama haujaikuta kuna link nimeiweka chini idownload manually uinstall
3.Register old number yako(uliyokuwa unaitumia mwanzo) kwa OGwhatsapp ,baada ya kumaliza njoo step ya 4
4.Install Official Whatsup(ile uliyo-unistall) then register na hiyo namba ya pili unayotaka kutumia kwenye device moja

Sunday, 26 June 2016

HISTORIA YA SANAMU LA MLINZI (POSTA)

 Sanamu (5)
Historia ya Mnara ule ilianza mwaka 1889, kisha, kabla na baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) hadi Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939 - 1945).
Kwa ufupi Sanamu ya mwanzo kukaa pale ni sanamu ya Herman Von Wissman, Gavana wa Kijerumani ambaye anakumbukwa kwa kutekeleza utekaji na mauaji ya Abushir Ibn Salim Al Harthi, mtawala/sultani
wa Pangani Tanga.

Haya hapa majina ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano na ufundi 2016


June 24 2016 Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ‘TAMISEMI’ imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2016. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali, Kwa urahisi zaidi unaweza kuyaona majina yote kwenye hii link hapa

Wednesday, 8 June 2016

Makadirio ya bajeti Kenya,Tanzania na Uganda yakamilika


Nchini kenya waziri wa fedha Henry Rotich leo amewasilisha bungeni bajeti ya makadirio ya matumizi ya pesa za serikali katika kipindi cha mwaka 2016-2017.
Bajeti hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 2.26 inatarajiwa kufadhiliwa kupitia ukusanyaji wa ushuru na mikopo kutoka kwa washirika wa kimaendeleo. Serikali inalenga kukopa shilingi bilioni 778 hatua ambayo itaongeza deni la kenya ambalo kufikia sasa ni shilingi trilioni 3.32.
Matumizi zaidi itaelekezwa kwa ujenzi wa miundo mbinu ikiwa ni pamoja ujenzi wa reli ya kisasa, kuimarisha usalama, huduma za afya na pia kuziwezesha serikali za majimbo.

Thursday, 26 May 2016

Tz:Madaktari Tanzania wafanya upasuaji wa kihistoria

UpasuajiMadaktari wamewafanyia upasuaji wagonjwa wawili

Madaktari wa Tanzania katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakishirikiana na wenzao wa India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa moyo wa aina yake Tanzania.
Upasuaji huo ujulikanao kama ‘bypass surgery’ ulishirikisha kupandikizwa kwa mishipa ya damu kutoka sehemu nyingine ya mwili moyoni bila kutumia mashine ya kusimamisha moyo na mapafu.
Kwa kawaida madaktari wanasema upasuaji wa moyo hufanyika baada ya moyo na mapafu kusimama, lakini upasuaji huo ulifanyika wakati moyo na mapafu vikifanya kazi.

Saturday, 2 April 2016

HATUA 10 ZA KUANZISHA BUSTANI YA NYUMBANI ( HOME GARDEN)

Habari za leo ndugu msomaji wa makala zetu, Tunatumai u mzima.
Kabla ya kuziangalia hizi hatua 10 za kuanzisha bustani yako nyumbani ni vyema tukaweza kujua umuhimu wa bustani ya nyumbani.
Amruth Home Garden is about a simple but innovative idea – to offer ___ 

 Beautiful home garden
Baadhi ya umuhimu wa bustani ya nyumbani ni pamoja na:
1. Kupata hewa safi na ya asili
2. Kupata sehemu nzuri ya kupumzikia nje ya nyumba.
3. Kupendezesha muonekano wa nje wa nyumba yako.
4. Kupangilia  na kuainisha matumizi ya ardhi ya nje.