Thursday, 9 January 2020

JINSI YA KUJIHIFADHIA MTAJI KWA AJILI YA KUANZISHA BIASHARA

    Picha inayohusiana
 Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika juu ya ukosefu wa ajira, lakini wanasahau kuwa ujasiamali ni jambo linalowezekana kabisa, kitu unachotakiwa kufanya ni kuanza kujihifadhia kidogo kidogo fedha kutokana na uwezo wako wa kifedha, unaweza kuanza na kiwango cha fedha kidogo kabisa kama shilingi mia moja ama mia mbili ili uweze kufikia malengo,kama itakuwa ngumu sana kwako kuhifadhi hela kwenye kibubu unaweza kufungua akaunti ya kuhifadhia hela katika benki yeyote ambayo itakuwa haina makato ya kiasi chochote cha fedha kutoka kwenye fedha yako uliyohifadhi, kwa mafano unaweza kufungua Fixed akaunti katika benki yoyote hii itakusaidia kuhifadhi hela kwa muda angalau wa mwaka mmoja utakuwa umepeta mtaji wa kuanzisha biashara yako.
 
   Njia nyingine ambayo unaweza kuhifadhi hela kwa ajili ya mtaji wa kuanzishia biashara ni kucheza mchezo, kwa ambao hawafahamu kuhusu mchezo huwa inakuwa hivi mnaweza kuwa watu wawili na kuendelea mnakuwa mnachangiana kiasi cha fedha kwa zamu kama msimu huu wewe ulimchangia mwenzako elfu mbili ndani ya siku tatu basi naye atakuchangia kwa kiasi hicho hicho.Hivyo mchezo unaweza saidia kwa kiasi kikubwa kupata mtaji wa kuanzishia biashara.

Biashara inawezekana kwa watu wa hali zote, haijalishi wewe ni masikini au tajiri cha msingi ni kutafuta fursa, kuzifanyia kazi, kutafuta mtaji, kuanza bishara na kusubiri mafanikio.

Imeandikwa na mzalendo mweusi

0 comments: